Friday, August 29, 2014

SHEIKH MWAHUTA ALEZEA MAZITO MSIKITI WA MSHINDO

Mwalimu wa Markazi ya
wamisri nchini Tanzania
tawi la Iringa, Kitanzini
Islamic Centre Sheikh
Salum Mwahuta jana
ijumaa alikhutubia
waislamu katika Msikiti wa
mshindo huko Iringa, na
kuzungumza mambo
mazito ambayo
mwanadamu aliyoneshwa
na Allah kabla ya kuja
kwake Duniani.

Sheikh Mwahuta katika
khutuba yake hiyo pamoja
na mambo mengine
alielezea pia namna ya
binadamu alivyoumbwa na
muda uliyopita kabla ya
kuletwa kwake hapa
duniani.

Sheikh Mwahuta kitalamu
ni mfasiri wa Qur-an
ambaye pia ni mtaalamu
wa somo la mirathi ya
kiislamu, mwahuta
alihitimu masomo yake
miaka kadhaa iliyopita
katika chuo kikuu cha
Azhar na kujipatia fani
mbali mbali kutoka kwa
marehemu Sheikh Twantwi
aliyekuwa sheikh Azhar
kipindi hicho.

Sheikh Mwahuta hutoa
khutuba za ijumaa katika
misikiti mbali mbali
mkoani Iringa ambapo ndo
makaazi yake yalipo kwa
sasa katika maeneo ya
Iringa Mjini Mtaa wa
Mwangota.

Khutuba ya Sheikh
Mwahuta inapatikana kwa
njia ya whatsapp tuma
inbox neno khutuba
ambatanisha na namba
yako ya whatsapp
utatumiwa kabla
haijawekwa online.

chini picha ya Sheikh
Mwahuta akiwa amemshika
mkono Sheikh Mohammed
Twantwi aliyekuwa Sheikh
wa Azhar kipindi hicho.

No comments: