Monday, May 5, 2014

SHEIKH ILUNGA HASSAN KUZIKWA LEO DAR

Sheikh ilunga Hassan Kapungu alifariki dunia jana usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya sukari na baadae figo kushindwa kufanya kazi.

Sheikh Ilunga amefariki katika jiji la Dar es Salaam, anatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Mwinyimkuu yaliyoko Magomeni Mapipa.

Maiti yake itasaliwa katika msikiti wa kichangani magomeni Dar es Salaam katika sala ya Alasiri saa kumi jioni.

Sheikh Ilunga ambaye alikwenda nchini India kwa matibabu aliwahi kukamatwa na polisi na kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kutoa mahubiri ya uchochezi, msiba wake upo Mbezi Goigi.

Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na amuingize katika pepo ya juu,aamin.

No comments: