Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amemfuta kazi waziri wake mkuu na kulivunja baraza lake la mawaziri Jumamosi(12.01.2013)akisafisha njia kwa kuteuliwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Serikali na waasi wa muungano wa Seleka , ambao walisonga mbele katika mashambulizi yao hadi karibu na mji mkuu Bangui mwezi uliopita, wamekubaliana kuunda serikali ya mpito mwishoni mwa mazungumzo yao yaliyofanyika katika mji mkuu wa Gabon , Libraville siku ya Ijumaa(11.01.2013).
"Kiongozi wa nchi, ameondoa matumizi ya amri iliyotolewa Aprili 22, 2011, inayohusiana na kuteuliwa kwa serikali," imesema amri ya rais iliyosomwa katika televisheni ya taifa. Soma Zai didw.de

No comments:
Post a Comment